Jinsi Ya Kupika Pilau

Jinsi Ya Kupika Pilau

Jinsi Ya kuandaa Pilau::Pilau ni chakula maarufu sana katika sehemu nyingi ulimwenguni. Aidha ni chakula kinachopendwa na kuenziwa na wengi, kwa rika tofauti tofauti si wakubwa wala wadogo wote hufurahia radha nzuri ya chakula iki. Bila shaka pilau inapendwa kutokana na sifa zake sufufu. Kwanza kabisa ni chakula chenye ladha marua. Vile vile ni chakula rahisi sana kutayarisha na kinachukua muda mchache sana kuwa tayari. Licha ya yote hayo, ni chakula kinachohitaji viungo vya kawaida sana vinavyopatikana katika soko lolote lile. Hapa tutakuonesha Jinsi Ya Kupika Pilau ya kuku au nyama kwa njia fupi na yakueleweka.

pilauPilau (Pilaf, palaw, pulao or polao) is a traditional, beautiful and fragrant rice dish made with many aromatic spices that add an incredible depth of flavor to the rice. It can be prepared with beef or chicken. Pilau has a great balance of flavors. It is a festive dish that is never lost during special occasions. It is made with rice cooked in well-marinated meat or chicken broth. Unlike Indian pilaf, the East African version does not use curry and is less spicy.

Ingredients -Jinsi Ya Kupika Pilau
MAHITAJI
1 Mchele (rice vikombe 3)
2 Nyama ya ng’ombe (beef 1/2 kilo)
3 Viazi mbatata (potato 3)
4 Vitunguu maji (onions 3)
5 Kitunguu swaum (garlic cloves 4)
6 Tangawizi iliyosagwa (ginger kiasi)
7 Hiliki nzima (cardamon 4)
8 Karafuu (clove 4)
9 Pilipili mtama (blackpepper 4)
10 Amdalasini (cirnamon stick 1)
11 Binzari nyembamba nzima(cumin seeds 1/2 ya kijiko cha chai)
12 Binzari nyembamba ya kusaga (ground cumin 1 kijiko cha chai)
13 Chumvi (salt)
14 Mafuta (vegetable oil)
15 Nyanya (fresh tomato 3)
16 Limao (lemon 1)
17 Pilipili (chilli 1)
18 Hoho (green pepper)
19 Njegere.

Jinsi Ya Kupika Pilau Steps By Steps

1 Marinate kuku/Nyama (weka siki na chumvi kwenye kuku umuache kwa takriban nusu saa)
2 Bandika sufuria motoni ueke mafuta, yakishika moto weka kitunguu ukikaange mpaka kiwe hudhurungi (golden brown)
3 Weka spices zote(dawa za pilau) pamoja na kitunguu thomu upike kwa sekunde kadhaa
4 Weka tomato, pilipili boga , karoti ,tomato  paste na kuku ufunike uache ziive kwa takriban dakika 10
5 Weka mchele uupike kwa sekunde kadhaa
6 Weka viazi na maji kiasi. funika mpaka maji yaelekee kukauka, takriban dakika 10(kiasi cha maji itategemea na mchele. Mimi nimetumia sunrice kwa hiyo nimeweka maji kiasi cha kufunika mchele na kuzidi kidogo)
7 Weka dania ukoroge vizuri na uyaache maji yakauke vizuri
8 kisha ufunike uweke moto mdogo kabisa kama unatumia gas cooker kwa takriban dakika 10_15(kama unatumia jiko la makaa weka moto wa juu na chini)
9 Pilau Itakua Teyari Kwa Kupakuliwa

Jinsi Ya Kupika Pilau

Ingredients -Jinsi Ya Kupika Pilau

EDITOR’S RECOMMENDATION

 

Michel John
Michael John is a founder of Superkwazulunews. He's inspired to share to the world his opinion on several small simple things that bring meaningfulness to life. He loves sports and spends most of his free time playing football and creating content, At various times, he has been the Social Editor, Creative Editor, and web editor
error: Content is protected !!