Tahasusi Mpya Kidato Cha Tano 2021

Tahasusi Mpya 2021

Serikali imetangaza kuanza kwa tahasusi (Combination) mpya tano kwa ajili ya Wanafunzi watakaoingia kidato cha tano mwaka 2021. Lengo la kuongeza tahasusi hizo ni kuondoa changamoto ya ukosefu wa wataalam nchini ambayo imekuwepo kwa muda mrefu. Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Seleman Jafo leo Jumatatu Machi 29, 2021 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Tahasusi Mpya
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi -Seleman Jafo

Tahasusi Mpya Kidato Cha Tano 2021

Zifuatazo ni Tahasusi Mpya Kidato Cha Tano 2021 zilizotangazwa kuanza kutolewa kwa wanafunzi wataojiunga na kidato cha tano

TAHASUSI MPYA MASOMO HUSIKA
PMC physics, Mathematics, and Computer
KFC Kiswahili, French and Chinese
KEC Kiswahili, English, and Chinese
PBF Physical Education, Biology and Fine Art
PGE Physical Education, Geography, and Economics

Jafo amesema tahasusi ya PMC itatolewa katika shule ya sekondari ya Dodoma ambayo itakuwa maalumu kwa wasichana ambapo kwa wavulana itakuwa sekondari ya wavulana ya Iyunga.

Amesema tahasusi ya KFC na KEC itatolewa katika shule ya sekondari ya wasichana Morogoro na ya wavulana Usagara wakati PBF na PGE itatolewa shule ya sekondari ya wasichana ya Makambako, shule ya sekondari ya wavulana Kibiti na sekondari ya Mpwapwa ambayo ni ya mchanganyiko.

Read Also

Michel John
Michael John is a founder of Superkwazulunews. He's inspired to share to the world his opinion on several small simple things that bring meaningfulness to life. He loves sports and spends most of his free time playing football and creating content, At various times, he has been the Social Editor, Creative Editor, and web editor
error: Content is protected !!